Privacy Policy

English / Swahili /
French /

SERA YA FARAGHA/USIRI YA TRIGGERISE Kuhifadhi data yako, usuri na data ya kibinafsi (jinsi ilivyoelezwa kwa Makala ya 4(1) ya kanuni za kijumla za ulinzi wa data (EU) 2016/679 (“GDRP”)) ni ya muhimu kwa Triggerise stitching na wahusika wake- Triggerise Kenya private limited, tawi la Triggerise Stitching Ethiopia, Triggerise India, Triggerise BV, Triggerise ya Afrika Kusini Pty limited na Triggerise LABS Unipessoal Lda (“sisi”, “yetu” ama “sisi”). Ni ya muhimu zaidi ya kwamba wateja wetu (“watumizi”) wanajihisi salama wakitumia huduma zetu, bidhaa na habari ambazo tunapeana kupitia kwa majukwaa yetu mbalimbali.

Sera hii inaonyesha msingi wa jinsi vile habari yoyote ya kibinafsi ambayo tunatoa kwako, ama ambayo unatupea itakavyo sindikwa/chakatwa. Tafadhali soma sera hii ya usiri kwa makini ili uelewe aina ya habari ambazo tunachukua kwako, jinsi tunavyozitumia, jinsi tofauti ambapo tutapeana kwa wahusika wa tatu, na haki zako kulingana na ile data ya kibinafsi unayotupea.

Unapotumia jukwaa, programu, tovuti zetu (“huduma”) utaombwa kuonyesha kukubali kwako kwa, na ikiwezekana, peana ruhusa yako kwa taratibu zilizoelezewa kwa sera hii.

SEHEMU YA 1 -SISI NI NANI Sera hii ya usiri inatumika kwa usindikaji wa data wa: Triggerise Stithcing na washiriki wake Kenya, Ethiopia, Portugal, Africa Kusini na Uholanzi.

Maswali, maoni na maombi juu ya sera hii ya usiri yanakaribishwa na yafaa kuelekezwa kwa privacy@triggerise.org​. Afisa wetu anayehusika na ulinzi wa data ni Admillo Ribeiro.

SEHEMU YA 2 - MTAZAMO WA KIJUMLA WA USINDIKAJI WA DATA UKIUNGANISHWA NA HUDUMA, BIDHAA NA HABARI. Habari unayotupatia. Utaombwa kutupatia habari zako wakati:

  • Wakati unajaza fomu katika tuvuti zetu, maombi yetu, vifaa vyetu vya kidigitali (kama facebook, Messenger, Twitter, Whatsapp, Instagram ama kuwasiliana nasi kupitia ujumbe mfupi, simu, barua pepe ama mengineyo)

  • Kujiandikisha/ kujisajili kutumia huduma, bidhaa ama ununuzi wetu, kujiunga na jarida letu, barua pepe za uendelezaji ama vifaa vingine vya masoko.

  • Kutumia huduma ama bidhaa unazopata kupitia majukwaa yetu

  • Kuweka kiwango kwa huduma ama bidhaa unazopata kwa majukwaa yetu.

  • Repoti shida kwa huduma ama bidhaa oliyopokea ama;

  • Kujaza utafiti wowote ama masomo ambayo tunatumia kwa minajili ya utafiti na kutathmini huduma zetu ama kuboresha ubora wa huduma ambazo tunawapatia.

Habari zile utaombwa kutupea kwa makusudi hayo yanaweza kuwa jinsia yako, tarehe ya kuzaliwa, namba ya simu, bidhaa ama huduma ulizopokea, mahali ambapo ulipokea bidhaa, huduma ama ujumbe, kukomboa tuzo ama habari nyingine yoyote inayohitajika kuhakikisha kitambulisho chako kama picha ya uso wako.

SEHEMU YA 3 -SHUGHULI MAALUM ZA USINDIKAJI, AINA NA KUSUDI LA UTUMIZI WAO. 3.1 UKITUMIA TUVUTI LETU Aina ya data in pamoja na: Anwani ya IP ya kifaa kinachotuma maombi, tarehe na wakati wa upatikanaji, jina na ULR ya ile faili inayotuma maombi, tovuti ambayo upatikanaji ulipatikana (“Referrer URL”) mtandao uliotumiwa na ikiwezekana, na mfumo wa uendeshaji wa kidude chako na kitambulisho cha anayekupa upatikanaji. Matumizi ya data hiyo: tunatumia hiyo data hapo juu kukuwezesha kupata tovuti yetu, kuhakikisha kwamba tovuti hiyo inaweza gundua uhusiano wa internet vyema n ani rahisi kutumia; kuchunguza mfumo wa usalama na uthabiti wake, na pia kuongezea kusudi la utawala.

Msingi wa kutumia: Mvuto ulio haki (Makala ya 6 (1) (f) GDPR) mvuto wetu wa haki unalingana na kusudi la kukusanya data ulivyoelezewa hapo juu. Hatutumii data ambayo inachukuliwa kwa kusudi la kukutambulisha. Haulazimishwi kupeana data ya binafsi hapo juu. Lakini, hautaweza kuingia kwenye tovuti kama habari kama hizo za kibinafsi hazitapeanwa.

Muda wa kuhifadhi: Data yako inatolewa baada ya siku 14, isipokuwa jambo lolote linalohusika na usalama litokee (kama kushambuliwa kwa DDoS). Kama kuna jambo lolote linalohusika na usalama, faili za usajili wa seva zinawekwa hadi hilo jambo linalohusika na usalama limemalizwa na kuelezwa kikamilifu.

3.2 UNAPOJISAJILI AMA KUJIANDIKISHA KUPOKEA HUDUMA AMA BIDHAA KWA MAJUKWAA AMBAYO TUNASIMAMIA Aina ya data ni pamoja na: Jinsia, tarehe ya kuzaliwa, picha y asura yako Matumizi ya data hiyo: tunatumia ujumbe huo hapo juu kukupa akaunti ya kutumia na upatikanaji wa huduma, bidhaa na habari ambazo tunapeana kwa majukwaa yetu. Haiwezekani kufikia huduma zetu kama (habari zisizo za hiari) hazijapeanwa.

Msingi wa utumizi: Utendakazi wa kandarasi ( Makala ya 6 (1) (b) GDPR/ ruhusa ( Makala 9 (2) (a) GDPR) Muda wa kuhifadhi: data yako inafutwa ama kutolewa vitambulisho (na haiwezi husishwa na mtu fulani) ukiomba akauti yako kufutwa. Kama akauti yako haifanyi kazi kwa Zaidi ya miezi 12, tutawasiliana nawe kuona kama ungependelea kuendelea kutumia huduma zetu. Ukiacha tena akaunti ya matumizi bila kutumiwa kwa miezi mingine 12, tutafuka akauti yako na kutoa vitambulisho kwa data yako (ili isiweze kuhusishwa na mtu yeyote).

3.3 UNAPOPOKEA HUDUMA, BIDHAA AMA HABARI KWA MAJUKWA AMBAYO TUNASIMAMIA Aina ya data ni pamoja na: Jinsia, tarehe ya kuzaliwa, picha y asura yako, aina ya huduma, bidhaa ama habari ambayo ulipokea, yule aliyekupa hiyo huduma ama bidhaa, tarehe uliyopokea hiyo huduma ama bidhaa ama habari, tathmini yako juu ya ubora wa huduma, bidhaa na habari ulizopokea, ikiwa unakomboa ari/mipango kama ya pointi za uaminifu (‘Tiko Miles’) na kama ni hivyo mahali unapokomboa ari/pointi za uaminifu na ari/pointi za uaminifu ulizotumia.

Matumizi ya data hiyo: Tunatumia ujumbe huo hapo juu kukupa upatikanaji wa huduma, bidhaa na habari ambazo tunapeana kupitia majukwaa yetu. Pia tunatumia ujumbe huo kuboresha idadi na ubora wa huduma, bidhaa na habari unazopokea kuthibitisha na kuhalalisha huduma, bidhaa na habari ulizopokea, kurejeshea wauzaji na watoa huduma kwa huduma, bidhaa na habari uliyopokea kutoka kwa majukwaa yetu, ili kutekeleza utafiti kama majaribio yaliyodhibitiwa bila utaratibu maalum, kutathmini ufanisi wa mwingilio wa utafiti, ili kuripoti kwa wafadhili wa huduma, bidhaa ama habari zilizo tolewa kwa majukwa yetu; ili kutekeleza utafiti wa watumiaji na kukufuatilia jinsi tunavyo weza kuboresha ubora wa huduma, bidhaa na habari ambazo unapokea kwa majukwaa yetu. Haiwezekani kupata huduma, bidhaa ama habari zetu kama habari zisizo za hiari hazijapeanwa.

Msingi wa utumizi: kandarasi ya utenda kazi (Makala ya 6 (1) (b) GDPR/ruhusa (Makala ya 9 (2) (a) GDPR) Muda wa kuhifadhi: Data yako inafutwa na kutolewa vitambulishi ( na haiwezi kuhusishwa na mtu yeyote) unpoomba akaunti yako kufutwa

3.4 MASOKO YA MOJA KWA MOJA KWAKO WA HUDUMA, BIDHAA AMA HABARI AMBAZO ZIKO KWA MAJUKWAA TUNAYO SIMAMIA. Aina ya data ni kama: : Jinsia, tarehe ya kuzaliwa, picha y asura yako, aina ya huduma, bidhaa ama habari ambayo ulipokea, yule aliyekupa hiyo huduma ama bidhaa, tarehe uliyopokea hiyo huduma ama bidhaa ama habari, tathmini yako juu ya ubora wa huduma, bidhaa na habari ulizopokea, , ikiwa unakomboa ari/mipango kama ya pointi za uaminifu (‘Tiko Miles’) na kama ni hivyo mahali unapokomboa ari/pointi za uaminifu na ari/pointi za uaminifu ulizotumia.

Matumizi ya data hiyo: tunatumia ujumbe huo hapo juu kukuza huduma, bidhaa ama kukupa habari ambazo tunaamini zitakuvutia. Unaweza rekebisha mipangilio yako ya masoko wakati wowote kwa aitha (1) kutuma ujumbe mfupi wa “KOMESHA” kwa nambari fupi uliyotumia kijiandikisha kwa huduma zetu (2) kuwasiliana na kueleza mobiliser aliyekusaidia kujiandikisha/ kujisajili kwenye majukwa yetu (3) kutupigia simu moja kwa moja kutumia namba walizokupa (4) kutuma ujumbe wa Whatsapp ama facebook ukisema “koma” ama (5) kututumia barua pepe.

Msingi wa utumizi: Ruhusa (Makala 6 (1) (a) GDPR) Muda wa kuhifadhi: Data yako inafutwa na kutolewa vitambulishi ( na haiwezi kuhusishwa na mtu yeyote) unpoomba akaunti yako kufutwa

3.5 KUTUMIA DATA INAYOAMBATANA NA AFYA YAKO KWA UTAFITI NA KUSUDI LA TAKWIMU Aina ya data ni kama: rekodi za bidhaa za afya ama huduma ambazo umepokea kutoka kwetu, ujumbe mwingine wa kiafya ambao umetupatia moja kwa moja ama kwa usahihi wakati wakutumia bidhaa ama huduma zetu. Utumizi wa data: Tunachakata data hii ili kufanya utafiti unaohusiana na utumizi na uchukuzi wa huduma na bidhaa za afya ya uzazi na kijinsia na kutayarisha ujumla wa takwimu wa utumizi wa bidhaa, huduma na habari za kiafya katika maeneo ambayo yaweza kulinganishwa na habari za idadi tulizonazo kukuhusu. Iwapo habari kama hizo zinawekwa hadharani, itawasilishwa kama takwimu zilizofupishwa na bila vitambulishi.

Msingi wa utumizi: Mchakato huo ni muhimu kwa utafiti wa kisayansi ama kwa kusudi la takwimu na tunachapisha takwimu zilizofupishwa na kutolewa vitambulishi ambavyo kutoka kwavyo ambapo kutambua mtu Fulani haiwezekani (Makala 9 (2) (j) DSGVO; sehemu 27 (1) BDSG). Mvutio wetu wa halali kwa kuchakata ujumbe kwa makusudi hayo ni kutoa repoti kwa wafadhili na wahisani wet una kwa kutoa repoti kwa wizara za afya na kuunga mkono uendelezaji wa huduma za afya kwa ujumla ambayo pia ni maslahi ya umma. Unaweza, kwa sababu zitokazo kwa hali yako Fulani, kata mchakato kama huo wakati wowote kwa kutuma barua pepe kwa privacy@triggerise.org

Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi wa ujumbe wako kwa msingi ambao tunatengeneza takwimu unalingana na wakati wa kuchataka kulingana na sehemu ya 3.2 unapoomba kufutwa kwa sehemu maalum ama unapofuta sehemu kwenye App, sehemu yako ya ujumbe haitatumiwa tena kwa makusudi hayo. Hizo takwimu hazina vitambulisho.

SEHEMU YA 4 - COOKIES NA KUFUATILIA KWENYE TUVUTI ZETU Tuvuti zetu hutumia “cookies”. Cookies ni faili za maandishi zilizowekwa kwenye kivinjari cha internet ama na kivinjari cha internet kwa kidude cha mtumizi (tarakilishi, tarakilishi kibao,ama simu).tunatumia jina “cookies” kurejelea vyombo vyote ambavyo vinakusanya ujumbe kwa tuvuti zetu (kama anwani ya IP, mahali na wakati wa kutembelea na mtumizi). Ujumbe wa mtumizi unaokusanywa hivi unatolewa vitambulishi. Ujumbe huo hauwekwi pamoja na habari zingine za kibinafsi za mtumizi. Mchakato huu unafanyika kwa msingi halali, itakikanavyo na sharia, kulingana na ruhusa yako.

SEHEMU YA 5 - TUNAWEKA WAPI UJUMBE WAKO WA KIBINAFSI Ujumbe wa kibinafsi ambao tunakusanya kutoka kwako unawekwa kwa muungano wa Ulaya kwa (Ulaya) seva za mawinguni za huduma za tovuti za Amazon EMEA S.A.R.L na kiti cha kibiashara huko Luxembourg. Lakini, ujumbe huo unaweza chakatwa na mchakato mdogo unaofanya kazi nje ya eneo la biashara la Ulaya (“EEA”) kwa msingi wa makubaliano ya mchakato wa ujumbe kama matakwa mengine ya makala ya 44 sehemu ya GDPR ya kuchakatwa kwa nchi za sehemu ya tatu yanalingana na kiwango kinachokubalika cha ulinzi kwa nchi ya tatu na kinakubalika kwa Makala ya 46 GDPR (kama kifungo cha kiwango cha ulinzi wa data, ama hali za kipekee chini ya Makala 49 GDPR).

Habari nyeti kati ya kivinjari chako na tuvuti yetu inhamishwa kwa hali fiche kutumia Transport Layer Security (“TSL”).unapopitisha ujumbe ulionyeti, ni lazima uhakikishe kila mara ya kwamba kivinjari chako kinaweza halalisha cheti chetu.

SEHEMU YA 6 - UFICHUZI WA UJUMBE WAKO WA KIBINAFSI Tunatumia wapeanaji wa huduma za kiufundi kuendesha na kudumisha huduma zetu, ambao ni wa msingi wa mchakato kwa makubaliano ya kuchakata data. Wapeanaji huduma ambao huchakata habari za kibinafsi kwa niaba yetu nje ya EEA (ama “chi za tatu”) watatumika tu kama mpokezi amepata uamuzi wa tume ya ulaya ya kukubalika ama inayofaa ama dhamana inayokubalika kwa hii nchi ya tatu ama ulinzi mwingine unaokubalika kuruhusu uhamishaji unapatikana chini ya sharia zinazokubalika. Kuongezea, hatuhamishi habari zako za kibinafsi kwa watu wa tatu- ila kwa kusudi yaliyotajwa kwa sehemu ya tatu hapo juu. Msingi wa utumizi: Msingi wa kisheria wa kuhamisha habari za kibinafsi kwa mchakato na usindikaji kwa processor unategemea msingi wa kisheria ambao sisi kama wanao dhibiti data tutategemea (ona sehemu ya 3 hapo juu)

Kama tunahitajika kwa msingi wa sharia za mitaa kwa maeneo ambayo sisi ama washiriki wetu hufanya kazi kufichua ama kuonyesha habari zako za kibinafsi.

Msingi wa utumizi: Wajibu wa kisheria

Tunaweza pia kushiriki ujumbe wako wa kibinafsi na washiriki wetu wa utafifi walioaminiwa ambao wanaweza chakata habari kwa niaba ya Triggerise kwa kusudi zilizotolewa hapa kwa hii sera ya usisri kwa kufuata makubaliano ya mchakato wa data uliokubalika ambao unapeana ulinzi kikamilifu wa habari zako za kibinafsi.

SEHEMU YA 7 -TUNAWEKA HABARI ZAKO ZA KIBINAFSI KWA MUDA GANI Tutaweka habari hiyo hapo juu kwa ule muda ambao ni muhimu ili kukupa huduma, kushughulikia jambo maalum ambalo laweza kuchipuka ama, vinginevyo, kama inavyohitajika kisheria ama mwili wa kuthibiti unaofaa. Wakati maalum wakuweka michakato tofauti mtawalia umeelezewa kinaga ubaga kwa sehemu ya 3 hapo juu.

Mradi tu akaunti yako ikikomeshwa, tutafuta habari zako za kibinafsi zinazohusiana na akaunti yako kwa muda wa mwezi mmoja.

Ikiwa habari zako za kibinafsi zimetumika kwa makusudi mbili tofauti, tutaiweka hadi kusudi ambalo lina muda mrefu liishe, lakini tutaacha kutumia kwa kusudi la muda mfupi punde tu muda mfupi ukiisha.

Tunazuia upatikanaji wa habari zako za kibinafsi kwa wale watu wanaotaka kutumia kwa makusudi inayofaa. Muda wetu wa kuweka unalingana na mahitaji yanayofaa ya kibiashara, na habari zako za kibinafsi ambazo hazihitajiki tena inaweza kutoleewa vitambulishi (habari zilizo tolewa vitambulishi zinaweza wekwa) ama ziharibiwe kwa usalama.

SEHEMU YA 8 - HAKI ZAKO Chini ya GDPR, unahaki kadhaa kulingana na habari zako za kibinafsi (kama ilivyotajwa hapo chini). Haki hizi zote zinaweza kutumika kwa kuwasiliana nasi kwa privacy@triggerise.org.

Haki ya kutoa ruhusa: una haki ya kuondoa ruhusa yako wakati wowote kwa kuwasiliana nasi kutumia barua pepe kwa anwani ifuatayo: privacy@triggerise.org ama kwa kutuma ujumbe mfupi kwa namba zozote fupi ambazo tunatumia kwa nchi ambazo tunafanya kazi. Kwa kuondoa ruhusa yako, uhalali wa mchakato kwa msingi wa ruhusa hadi pale ambapo unatoka hautaathirika.

Haki ya kupinga: una haki ya kupinga chini ya sharia za Makala ya 21 DSGVO. Utapata habari Zaidi hapo chini:

  • Haki ya kukataa iwapo mchakato una msingi wa mvuto wa kisheria: kama mhusika wa data, una haki ya kupinga kwa madai yanayohusika na hali Fulani kwa wakati wowote kuchakata habari zako za kibinafsi ambayo ina msingi wa Makala ya 6 (1) (e) ama (f) GDPR, ikiwamo ufichuzi kwa msingi wa utoaji. Ikiwa kutakuwa na kukataa inayoambatana na hali yako Fulani, hatuwezi kuchakata habari zako za kibinafsi hadi tuweza kupambanua sababu za kisheria za kuchakata ambazo zinapita mvuto wako, haki na uhuru ama kwa kutekeleza, kufanya ama kinga kwa madai ya kisheria.

  • Haki ya kupinga penye tunachakata habari zako za kibinafsi kwa makusudi ya takwimu: Tukichakata habari zako za binafsi kwa makusudi ya takwimu kulingana na Makala 9 (2) (j) DSGVO sehemu ya 27 (1) BDSG, una haki ya kukataa mchakato kama huo kwa sababu zinazotoka kwa hali yako Fulani. Ikiwa kuna kukataa kama hiyo, hatutachakata tena habari za kibinafsi zinazohusika na kusudi hiyo isipokuwa kama kuchakata ni kwa muhimu kutekeleza jukumu ambalo lina maslahi ya umma, ama kukomesha kuchakata inaweza fanya kutowezekana ama kuzuia kupata makusudi ya takwimu na kuendelea kuchakata ni muhimu kwa kutekeleza makusudi ya takwimu.

  • Haki ya kukataa masoko ya moja kwa moja: habari zako za kibinafsi zikichakatwa kwa makusudi ya masoko ya moja kwa moja, una haki ya kukataa wakati wowote kuchakatwa kwa habari zako za kibinafsi kwa masoko kama hayo, imbayo inahusu kuficha hadi ambapo inahusiana na masoko ya moja kwa moja kama hayo. Ukipinga mchakato kwa masoko ya moja kwa moja, hatuchakati tena habari zako za kibinafsi kwa makusudi haya. Kutumia haki zako za kukataa, unaweza wasiliana nasi wakati wowote kwa kutuma barua pepe kwa privacy@triggerise.org

Haki ya kupewa taarifa: kama mhusika wa habari, una haki ya kupokea upatikanaji na habari chini ya hali zilizopeanwa kwa Makala 15 GDPR. Hii inamaanisha uko na haki ya kupata uthibitisho kutoka kwetu ikiwa tunachakata habari zako za kibinafsi. Kama ni hivyo, uko na haki pia ya kupata upatikanaji kwa habari za kibinafsi na habari zilizo katika Makala 15 (1) GDPR. Hi ni pamoja na habari zinazohusu makusudi ya mchakato, makundi ya habari za kibinafsi ambazo zinachakatwa na wanaopokea ama makundi ya wanaopokea ambao habari zao za kibinafsi zimefichuliwa ama zitafichuliwa.

Haki ya kufutwa/ haki ya kusahauilika: Kama mhusika wa data, una haku ya kufutwa (haki ya kusahaulika) chini ya hali zinazopeanwa kwa Makala 17 GDPR. Hii inamaanisha ya kwamba kwa ujumla una haki ya kupokea kutoka kwetu kufutwa kwa habari zako za kibinafsi tunatakikana kufuta habari zako za kibinafsi bila kuchelewa kwokwote ikiwa sababu yeyote ambayo imenakiliwa kwa Makala 17 (1) GDPR inahusika. Unaweza fanya hivyo kwa kufuta akaunti yako wakati wowote. Kama tumefichua habari zako za kibinafsi na tunahitajika kufuta, pia tunatakikana, tukizingatia hali ya ufundi iliyoko na gharama ya ketenda, kuchukua hatua zinazofaa ikiwamo hatua za kiufundi, kuwajulisha wathibiti ambao wanachakata habari hizo za kibinafsi ambazo umeomba zifutwe na wathibiti kama hao wa viungo, ama nakala ama zinazofanana na hizo habari za kibinafsi (Makala 17 (2) ya GDPR). Haki ya kufutwa (haki ya kusahaulika) haitumiki kwa kipekee kama mchakato ni wa muhimu kwa sababu ya sababu moja wapozilizo peanwa Makala 17 (3) GDPR. Hii inaweza kuwa kwa mfano kama mchakano ni wa muhimu kwa kufuata hitaji la kisheria ama kwa kuthibiti ama kujukinga na madai ya sharia (Makala 17 (3) (b) na (e)) GDPR

Haki ya kizuizi cha mchakato: Kama mhusika wa data, una haki ya kizuizi cha mchakato chini ya hali zilizopeanwa kwa Makala 18 GDPR. Hii inamaanisha kwamba una haki ya kupokea kutoka kwetu kizuizi cha mchakato kama hali moja wapo iliyopeanwa kwa Makala 18 (1)GDPR inahusika. Hii inaweza kuwa kwa mfano ukipinga uadilifu wa habari za kibinafsi. Kwa hali kama hiyo, kizuizi cha mchakato kinadumu kwa muda ambao unatuwezesha uadilifu wa habari za kibinafsi (Makala 18 (1) (a) GDPR). Kizuizi kinamaanisha ya kwamba habari za kibinafsi zilizowekwa zinasahihishwa kwa minajili ya kuzuia kuchakatwa katika siku za usoni (Makala 4 nambari 3 GDPR).

Haki ya uwezo wa kubeba data: Kama mhusika wa data, una haki ya uwezo wa kubeba data chini ya hali zilizopeanwa kwa Makala 20 GDPR. Hii inamaanisha ya kwamba kwa ujumla una haki ya kupokea habari zako za kibinafsi ambazo ulitupa kwa mpangilio, unayotumika kwa urahisi na kwa hali inayoweza kusomwa na mashine na kupitisha habari hizo kwa mthibiti mwingine bila kizuizi chochote kutoka kwetu kama mchakato una msingi wa ruhusa kulingana na Makala 6 (1) (a) ama Makala 9 (2) GDPR ama kwa kandarasi kulingana na Makala 6 (1) (a) GDPR na mchakato unafanywa kwa kujiendelesha wenyewe (Makala 20 (1) GDPR). Kwa kuhusika kwa haki yako ya uwezo wa kubeba data, pia una haki kiujumla ya kupitisha moja kwa moja kutoka kwetu hadi kwa mthibiti mwingine kama inawezekana kiteknologia (Makala 20 (2) GDPR).

Haki ya kurekebisha: Kama mhusika wa data, una haki ya kurekebisha chini ya hali zilizopeanwa kwa Makala 16 GDPR. Hii inamaanisha kwa umaalum una haki ya kupokea kutoka kwetu bila kechelewa kokote urekebishaji wa kutokuwa na usahihi katika habari zako za kibinafsi na kumalizia habari za kibinafsi ambazo hazikuwa kamilifu. Haki ya kulalamika: Kama mhusika wa data, una haki ya kuweka malalamishi kwa mamlaka ya usimamizi chini ya hali zilizopeanwa kwa Makala 77 GDPR. Mamlaka ya usimamizi ambayo inatusimamia ni XXXX Kutuomba kuacha kuchakata habari zako za kibinafsi ama kufuta habari zako za kibinafsi huenda ikamaanisha kwamba hauwezi tena kutumia huduma, bidhaa ama habari ambazo zinahitaji kuchakatwa kwa aina ya habari za kibinafsi ambazo umetuomba kufuta, ambayo matokeo yake ni kwamba hauwezi tena kutumia huduma, bidhaa ama habari.

SEHEMU YA 9 - MABADILIKO KWA SERA HII Mabadiliko yoyote tunayofanya kwa sera yetu ya usiri katika siku za usoni itawekwa kwa ukurasa huu, na iwapo sawa, utajulishwa kwa ujumbe mfupi, barua pepe ama taarifa nyingine. Kwa hivyo tunakupa moyo uipitie mara kwa mara ili uwe na ufahamu jinsi tunavyochakata habari zako.

We use cookies to understand how you use our website and improve your experience. Read more about this. Okay, I accept